وبلاگ بلیان

WESTMINSTER SHORTER CATECHISM IN SWAHILI (KATEKISIMU FUPI) 1

معرفی کتاب «WESTMINSTER SHORTER CATECHISM IN SWAHILI (KATEKISIMU FUPI) 1» نوشتهٔ Daniel J. Seni، منتشرشده توسط نشر Moccony Printers در سال 2020. این کتاب در فرمت pdf، زبان sw ارائه شده است.

Katekisimu [κατηχέω] ni neno la Kigiriki lenye maana ya kufundisha kwa mdomo kwa mfumo wa maswali na majibu. Ni njia ambayo tangu zamani ilitumiwa kwa ajili ya kufundisha kwa muhtasari imani ya Kikristo. Tumelazimika kutoa ufafanuzi mfupi ili kupinga majaribio ya wazushi ambao hulaghai washirika kwa madai kwamba Katekisimu iko kidini sana, na siyo kiroho, madai ambayo hayana ukweli wowote. Watumiaji wanapaswa kujua kwamba Katekisimu hii imesheheni mafundisho ya msingi ya Ukristo kwa kuzingatia Biblia Takatifu. Kuna aina kuu mbili za Katekisimu za Westminister; Katekisimu fupi na Katekisimu ndefu. Katekismu fupi ina maswali 107 na Katekisimu ndefu ina maswali 196. Hii ni Katekisimu fupi ambayo ilianza kuandikwa mwaka 1646 na kumalizika mwaka 1647. Iliandaliwa na sinodi ya wanatheolojia Warefomati wa Uingereza na Scotland. Makanisa mengi ya “Ki-Refomati” (Reformed Churches), yakiwemo makanisa ya Ki-Presibiteriani hutumia Katekisimu hii. Hivyo basi, dhima yetu ni kuhakikisha kwamba washirika wote wanafundishwa misingi ya imani ya Kikristo kwa kuzingatia Katekisimu hii. Na kwamba baada ya kumakinika katika Katekisimu fupi, pia wawe tayari kumakinika katika Katekisimu ndefu. Tafsiri hii imetokana na toleo la Kiingereza cha Kisasa, na hivyo tumejaribu kuzingatia maneno-msingi na tahajia yake, na pia tumejaribu kwa umakini kuzingatia maana ya awali. DANIEL JOHN SENI Yaliyomo 1. Kusudi la Maisha na Maandiko Matakatifu (Swali 1-3) 2. Mungu Mmoja na Utatu (Swali 4-6) 3. Mpango wa Mungu wa Milele (Swali 7-8) 4. Uumbaji (Swali 9-10) 5. Maongozi ya Mungu (Swali 11- 12) 6. Dhambi katika Jamii ya Wanadamu (Swali 13-19) 7. Agano la Mungu la Neema (Swali 20) 8. Kristo Mpatanishi: Nafsi na asili ya Mpatanishi (Swali 21-22) 9. Kristo Mpatanishi: Ofisi tatu za Kristo (Swali 23- 26) 10. Kristo Mpatanishi: Hali ya Kristo ya kujishusha (Swali 27) 11. Kristo Mpatanishi: Hali ya kuinuliwa kwa Kristo (Swali 28) 12. Wito wa Mungu wenye ufanisi (Swali 29-31) 13. Faida katika maisha haya (Swali 32) 14. Faida katika maisha haya: Kuhesabiwa haki (Swali 33) 15. Faida katika maisha haya: Kufanywa Wana (Swali 34) 16. Faida katika maisha haya: Utakaso (Swali 35) 17. Faida nyinginezo: a. Katika maisha haya (Swali la 36) b. Wakati wa kifo (Swali la 37) c. Wakati wa ufufuo (Swali la 38) 18. Sheria ya Maadili (Swali 39-40) 19. Sheria ya Maadili: Muhtasari Wake (Swali 41-42) 20. Sheria ya Maadili: Ufafanuzi wa amri kumi (Swali 43-81) 21. Sheria ya Maadili: Makosa na Adhabu (Swali 82-84) 22. Amri ya Mungu katika Injili (Swali 85) 23. Amri ya Mungu katika injili: a) Imani (Swali la 86) b) Toba iletayo Uzima (Swali 87) 24. Njia za Neema (Swali 88) a) Neno la Mungu (Swali 89-90) b) Sakramenti (Swali 91-93) i. Ubatizo (Swali 94-95) ii. Meza ya Bwana (Swali 96-97) 25. Maombi (Swali 98-99) 26. Ufafanuzi wa Sala ya Bwana (Swali 100-107)
دانلود کتاب WESTMINSTER SHORTER CATECHISM IN SWAHILI (KATEKISIMU FUPI) 1